October 2022
Matangazo ya Usharika tarehe 30/10/2022
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 30 OKTOBA, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
MATENGENEZO YA KANISA, USHUHUDA WETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 23/10/2022
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
Baraza la Wazee wa Kanisa 2022 - 2026
Hii ni orodha ya Baraza Jipya la Wazee wa Kanisa wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral. Baraza hili jipya lenye jumla ya wajumbe 33 ambao wamepatikana baada ya kufanyika uchaguzi na hivyo wajumbe hao kupigiwa kura nyingi na washarika wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front mnamo mwezi Agosti 2022.
Kwa mujibu wa Katiba ya KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front, wajumbe hawa watahudumu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2022 mpaka 2026.
Luka 17:11-19 - 28-10-2022
Matendo 14:8-13 - 27-10-2022
Luka 18:38-43 - 26-10-2022
Matendo 9:32-35 - 25-10-2022
Matangazo ya Usharika tarehe 23/10/2022
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 23 OKTOBA, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
IMANI YAKO IMEKUPONYA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 16/10/2022
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Luka 7:2-12 - 24-10-2022
Luka 4:30-31 - 21-10-2022
Usharika wafanya Semina kwa Baraza Jipya la Wazee
Siku ya Ijumaa, tarehe 14 Octoba 2022 ilifanyika semina ya siku moja kwa Baraza Jipya la Wazee wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral. Semina hiyo iliyolenga kuweka mipango na mikakati itakayoongoza baraza hilo katika utendaji wake wa kazi za kila siku iliongozwa na Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk Alex Malasusa.
Usharika Waadhimisha Sikukuu ya Mikael na Watoto 2022
Kama ilivyoainishwa katika kalenda ya KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Jumapili ya tarehe 2 Oktoba 2022 Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral uliadhimisha Sikukuu ya Mikael na Watoto.
Sikukuu ya Mikael na watoto hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kumkumbuka malaika Mikel na watakatifu wote pamoja na watoto. Ibada hii hufanyika kwa kuongozwa na watoto wakisaidiana na walimu wao pamoja na mtumishi wa usharika (parish worker).
