SALAAM ZA KRISMASI 2018...CHRISTMAS GREETINGS 2018

 
[To view in English http://www.azaniafront.org/node/886/]

 Nawe Bethlehemu,katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumba ya Yuda;

Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli. “. Mathayo 2:6

Ninakusalimu kwa niaba na Chaplain Rev Charles Mzinga na Baraza la Wazee na kuwatakia wote Kristmasi njema na Mwaka Mpya.

Yesu Kristo  amezaliwa Haleluya!   Tunamshukuru Mungu kwa zawadi kuu. Ametupa zawadi ya Yesu Kristo Mwokozi wetu. Tunakumbuka jinsi alivyozaliwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita kule Israeli katika mji ndogo wa Bethlehemu karibu na jiji la Yerusalemu.

Mstari ulitotajwa hapo juu, Mtume Mathayo aliandika katika Injili yake. Ni nukuu kutoka nabii Mika. Mika alitabiri kuwa mtawala atatoka Bethlehemu. Wakati Mamajusi walipofika kutoka mbali wakifuata nyota walifika kwa Mfalme Herode. Walimwuuliza  Herode  “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi”?  Mfalme Herode aliwaita viongozi wa dini na kuwauliza Kristo kazaliwa wapi? Ndiyo hawa Makuhani na waandishi walijibu kwa kunukuu Nabii Mika kwamba anapaswa kuzaliwa Bethlehemu..    

Tunamshukuru Mungu kwamba Yesu Kristo ni mwana wa Mungu aliyekuja duniani kutuokoa. Yesu alitimiza maandiko yote. Yesu alikuja duniani kama Myahudi lakini alikuja kwa watu wote duniani, watu wa kila kabila na kila lugha na kila taifa. Njooni kanisani tusherehekee pamoja ujio wa Mwokozi wetu.

                                                                                                ....../Pastor P. Chuwa

Karibuni katika ibada zetu zifuatazo:

IBADA ZA KRISTMASI  NA MWAKA MPYA (KISWAHILI)

  • Jumapili tarehe 23 Disemba Ibada ni saa 1 na saa 3.30 asubuhi
  • Jumatatu tarehe 24 Disemba, Usiku Mtakatifu ibada inaanza saa 1.00 usiku hadi saa 3.00 usiku
  • Jumanne tarehe 25 Disemba, Siku ya Kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Saa 1.00 na saa 3.30 asubuhi
  • Jumatano tarehe 26 Disemba ibada ni moja saa 2.00 asubuhi pamoja na Ubatizo na Kipaimara, 
  • Jumapili tarehe 30 Disemba ibada ni saa 1.00 na saa 3.30 asubuhi
  • Jumatatu tarehe 31 Disemba Siku ya Mwisho wa Mwaka, ibada ni saa 1.00 hadi saa 3.00 usiku
  • Mkesha  wa mwaka mpya utaanza mara baada ya ibada ya saa 1:00 usiku hadi alfajiri siku ya Jumanne tarehe 1 Januari 2019
  • Jumanne tarehe 1 Januari 2019 , Mwaka Mpya ibadi ni saa 2.00 hadi saa 4.00 asubuhi ni pamoja na kushriki Chakula cha Bwana.

KARIBUNI WOTE TUMWABUDU MUNGU WETU KWA PAMOJA